Pages

Friday, November 2, 2012

WENGER: VAN PERSIE ALIKATAA MSHAHARA WA £300,000 ZA CITY NA KUICHAGUA MAN UNITED



Rocking Robin: Van Persie has already scored nine goals for Manchester UnitedRobin van Persie alikataa ofa nzito ambayo inakadiriwa kufikia £300,000 kwa wiki utoka kwa Manchester City  kabla hajaamua kujiunga na mahasimu wao Manchester United, hiyo ni kwa mujibu wa kocha Arsene Wenger.
Van Persie ameendeleza makali yake ambayo msimu uliopita yalimfanya afunge mabao 37 akiwa na Arsenal na sasa akiwa na United tayari ameshatupia mabao tisa katika mechi 12.

Lakini magoli hayo yangeweza kuwa kwa ajili ya timu inayovaa jezi za blue kutoka jiji la Manchester badala ya United, baada ya Mholanzi huyo kukataa kujiunga na City, ingawa Wenger amegoma kutaja sababu iliyomfanya RVP aitose City.

Kwa hakika zaidi inaonekana haikuwa kwasababu ya masula ya fedha, kwa kuwa City walitoa ofa ya mshahara wa £300,000 kwa wiki.
Van Persie hapati kiasi hicho pale Old Trafford, ingawa hiyo ndio fedha ambayo inatajwa Wayne Rooney amekuwa akilipwa -ingawa United wamekanusha hilo.

'Ni kweli Manchester City walikuwa wakimtaka Van Persie na akaamua kuchagua kujiunga na United," alisema Wenger akiongea na gazeti la Independent.

'Hakunipa sababu za kuikataa City lakini na mie sikutaka kujua zaidi kuhusu hilo.
'Je inaniumiza kumuona akiondoka hapa na kwenda kwenye klabu nyingine ya hapa Uingereza? Kwa kweli hilo sio jambo nililotaka!
'Ninatumaini mapokezi yake atakapocheza nasi hayatokuwa mabaya kwa sababu ameichezea klabu yetu kwa miaka nane. Ningependa aheshimiwe.
Remember me? Arsene Wenger's (left) Arsenal will face his former striker on Saturday for the first time since he joined United for £24m in the summer


'Unadhani nashangazwa na mafanikio anayoyapta pale United? Hapana, pale Manchester anazungukwa na wachezaji wazuri, na Robin na hatari mno ndani ya box." - Wenger

No comments:

Post a Comment