Pages

Friday, November 2, 2012

MESSI: "NI KWELI NILIGOMBANA NA VILLA, LAKINI SASA TUPO SAWA"



Mshambuliaji wa Barcelona  Lionel Messi ameamua kufunguka na kuweka sawa kwamba hana matatizo yoyote na David Villa.
Wawili hao walitoleana maneno makali wakati wa mechi uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Barcelona na Granada mapema msimu huu, na vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba wawili hao wamekuwa na mahusiano mabovu tangu kutokea kwa tukio hilo.

Jaokuwa Messi amekuja kuweka wazi kwamba tofauti zao ziliishia pale pale uwanjani.

"Ishu ile ilileta mtafuruku kiasi baada ya tukio lile kutokea. Lakini kwa hakika ugomvi ule uliishia pale uwanjani," Messi alikaririwa akisema kupitia gazeti la El Mundo Deportivo. "Sasa hatuna tofauti zozote tunapatana kama zamanina kama ilivyo kwa watu wengine kwenye chumba cha kubadilishia nguo."

Aliongeza, "David ni mtu mzuri ambaye hagombani na mtu yoyote. Ni vigumu sana kugombana na mtu mwenye tbia kama zake.

"Tuliongea kuhusu kilichotokea, na kwa hakika hatuna tofauti zozote kwa sasa." - Alimaliza Messi.

No comments:

Post a Comment