Pages

Monday, November 26, 2012

YANGA KWENDA NCHINI UTURUKI KUJIANDAA NA RAUNDI YA PILI YA VPL.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb , ametoa taarifa kwa vyombo vya habari leo hii kuelezea mambo makuu mawili : - 

1.Maendeleo ya timu katika ligi kuu ya Vodacom
2.Mipango ya kuendelea kufanya vizuri

Dondoo ni kama ifuatavyo : - 
Tangu kuingia madarakani kwa uongozi wa sasa Julai 15 mwaka huu ni takribani miezi mitano (5), imeshapita, timu ya Yanga imecheza jumla ya michezo  23, imeshinda michezo 19, sare michezo miwili (2), imefungwa michezo mitatu (2).
 
 - Timu ya Yanga imefunga jumla ya mabao  52 katika michezo yote, imefungwa mabao 14 katika michezo yote tangu mwezi July 2012.
 - Mpaka sasa ktk ligi kwa Yanga ina pointi  29, imefunga mabao 25 na kufungwa mabao 10

 - Kocha Mkuu Ernie Brandts amewapandisha wachezaji watatu kutoka timu ya vijana ya U-20 ambao ni ni mshambuliaji George Banda, kiungo wa pembeni Rehani Kibingu na golikipa Yusuph Abdul.
 - Kikosi cha timu ya vijana tangu mwezi July kimecheza jumla ya michezo 24 ya kirafiki na mashindano, kikiwa imeshinda michezo 20, imetoka sare michezo mitatu (3) na kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya U-20 Ruvu Shooting.

 - Timu imeanza mazoezi rasmi leo asubuhi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kombe la Kagame mwezi januari 2013

 - Kamati ya mashindano baada ya kukaa na kujadiliana na kocha, kwa pamoja tumeamua timu itakwenda kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kipindi cha wiki mbili, safari ya Uturuki itakua ni mara tu baada ya sikukuu ya X-mass kabla ya mwaka mpya. Hii itatoa fursa kwa wachezaji wote kuweza kujumuika pamoja kwani kwa sasa baadhi ya wachezaji wetu wapo wanazitumikia timu zao za taifa kwenye mashindano ya Chalenji nchini Uganda.

- Timu ikiwa nchini Uturuki inatazamiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu mbili ambazo zitajulikana baadae na tutawajulisha kabla ya kuondoka.
Kocha Brandts anaangalia sana Nidhamu ndani na nje ya uwanja, kwani anaamini nidhamu ndio msingi wa timu kufanya vizuri.

 - Kocha anapenda kila mchezaji awe na malengo, na si kucheza mpira tu pasipokuwa na malengo, Lazima mchezaji ajue kabla ya kuwaza kucheza soka nje ya nchi inampasa kupigania kuhakikisha anapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu yake.

- Kuhusu Usajili kocha ametuletea mapendekezo yake, tunayafanyia kazi na muda ukiwa tayari tutawajulisha, maana dirisha dogo la usajili linafungwa disemba 15 hivyo bado tuna siku zaidi ya 20.
 
Hatupendi masuala ya kukurupuka kutangaza vitu ambavyo havijakalmilika, ndio maana hata usajili wetu uliopita tulitangaza baada ya kukamilisha kila kitu.
Hayo ndo machache niliyotaka kuwajulisha ndugu zangu waandishi wa habari.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
 
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano na usajili
 
...

No comments:

Post a Comment