Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedict wa 16.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Benedict wa 16 amejiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter.
Baba Mtakatifu alifungua ukurasa huo kwa lugha ya Kiingereza ambao tayari umekwisha wavutia watu 92,000.
Idadi hii inatarajiwa kuongezeka mara kiongozi huyo mzaliwa wa Ujerumani atakapoandika kitu kwenye ukurasa huo.
Bado hajasema chochote hadi sasa tangu kuufungua.
Uongozi wa Vatican umesema kuwa ataanza kuutumia rasmi tarehe 12 mwezi huu.
You might also like:
No comments:
Post a Comment