Mafundi wakivunja Nyumba iliyokuwa katikati ya Barabara baada
ya mmiliki wa nyumba hiyo kukubali fidia ya 260,000 yuan ($41,000)
nyumba hiyo ilikuwa imebaki yenyewe katikati ya barabara ya Wenling
huko katika Jimbo la Zhejiang na kubomolewa Dec. 1, 2012.
Pichani ni nyumba hiyo ambayo wameliki wake walikataa kuivunja
wakipinga kupewa malipo kiduchu ya fidia hivyo nyumba hiyo kubaki
peke yake na katikati ya Barabara.
Kutoka katika Kijiji cha Xiayangzhang chifu Chen Xuecai alisema
kwamba nyumba hiyo imevunjwa Jumamosi baada ya mmiliki
wake mkulima Luo Baogen na mke wake, kukubali
kupokea fidia ya yuan 260,000($41,000).
Luo, mwenye 67, alikuwa ndio ametoka kumaliza kujenga
nyumba yake kwa gharama ya Yuan 600,000($95,000) wakati
serikali ilipokuja na kumuambia kuwa watamlipa fidia ya Yuan
220,000 ($35,000) kuondoka kwenye nyumba hiyo na Bwana
Luo akagoma malipo hayo akidai ni madogo kulinganisha na
gharama aliyotumia kuijenga nyumba hiyo.Baadae wakapandisha
fidia hiyo hadi Yuan 260,000($41,000) wiki iliyopita na kukubalika
baada ya kukutana na maafisa wa Serikali.
No comments:
Post a Comment