NEW YORK, Marekani
VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo.

Taarifa
hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya kumfanya mwanamke awe laini,
video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na
kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini)
baada ya muda mfupi.
Imebainika
kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa makalio ya akina dada
kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya binadamu.
Wataalamu
wa mambo wanadai kwamba pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa
huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika mpangilio usio
sahihi.
Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa saratani.
Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu".

Anaongeza:
"Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi. Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa
haya makalio yangu yote kwa sasa." alisikika akisema.
Mpaka
kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa katika mtandao wa kijamii wa
Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu 278,000 wanaotembelea huku
ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000 wakipeleka katika kurasa zao.
Mtumiaji
mmoja wa mtandao huo kutoka nchini Marekani Donna Wright-Levy,
alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda maeneo kadhaa ambako
hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina ulazima wa kwenda
kupima saratani".
Ni vigumu
kuthibitisha mwanamke huyu alitumia kliniki gani wakati alipofanyiwa
uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake miaka miwili iliyopita.
Lakini
mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya upasuaji ya BAAPS Aurora nchini
Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni mshauri wa upasuaji anaamini
kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho ya makalio yake kwa dawa za
silicone.
Alisema
tatizo hutokea wakati nyama ya makalio inaposhindwa kuulinda vema mwili
na kuwa imara katika nyama na mifupa na hivyo madhara huanza kutokea juu
ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya nyama na baadaye mfupa.
Ni
matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji ya dawa za kuongeza
ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni lazima itokee baada ya
muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina maana wakati wake ukiisha
kitarudi kama awali.
"Huyu
mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma na kwa juu zaidi hivyo
tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana hakufanya upasuaji
bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema Richards.
Soma zaidi Habari Hii: http://www.mwananchi.co.tz
Soma zaidi Habari Hii: http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment