ATAKATA ICHUKUE HATUA MADHUBUTI DHIDI VYA VIKUNDI VYOTE CHOCHEZI
WAKATI
baadhi ya vinara wa vurugu zinazohusishwa na masuala ya kidini wakiwa
Mahakamani jijini Dar es Salaam na Zanzibar, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex
Malasusa ameidai kuwa Serikali ina kigugumizi katika kusema ukweli
kuhusiana na vurugu hizo na zingine zinazotokana na imani za kidini
nchini.
Akihutubia
wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa 31 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani
unaofanyika mjini Bagamoyo jana, Askofu Malasusa alisema kuwa,
Serikali ilipaswa si tu kuwakamata, bali pia kufuta usajili wa vikundi
vyote vinavyosababisha vurugu nchini.
Askofu
Malasusa alisema kuwa, kitendo cha Serikali kukaa kimya bila kuchukulia
hatua vikundi vilivyosajiliwa na kuwa na mlengo tofauti na madhumuni
yake ama inapendezwa, kuvutiwa na hata kushawishiwa na yale ambayo
yanazungumzwa na vikundi hivyo japo wanaweza wasikubaliane na vitendo
vyao.
Kuanzia
katikati ya Oktoba mwaka huu, kulizuka ghasia katika mji wa Zanzibar na
vitongoji vyake zinazodaiwa kufanywa na wafuasi wa Kikundi cha Uamsho
vilivyokwenda sambamba na kuchoma makanisa.
Katika
mfululizo wa matukio hayo, makanisa takriban saba yalichomwa moto jijini
Dar es Salaam baada ya kuzuka ghasia maeneo ya Mbagala, wilayani
Temeke, zilizotokana na imani za kidini na watu 49 walikamatwa na
baadaye kuachiwa huru.
Hata
hivyo, kesi bado ziko mahakamani kwa viongozi wa wafuasi hao ambao kwa
Zanzibar ni Farid Hadi Ahmed na Dar es Salaam, Sheikh Ponda Issa Ponda.
“Naomba
serikali ipige marufuku vikundi hivi, hatutaki viendelee wala kupewa
nafasi kushamiri hata kama ni ndani ya kanisa ninaloliongoza kwani
yaliyotokea Rwanda na Burundi na hata Kenya. hatutaki yatokee hapa
kwetu” alisema Askofu Malasusa.
Mkuu huyo wa Kanisa alisema katika hotuba yake ya ufunguzi kuwa, pamoja Wakristo wamejifunza kupitia maandiko Matakatifu kuwa: ‘Kushindana kwetu sio kwa juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, majeshi, pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’, hana uhakika kama wote wana uvumilivu wa kutosha.

“Sina
hakika mtu akija na silaha kushambulia na wewe upo ndani na silaha na
biblia kama utatoka na biblia, au silaha,” alisema Mkuu huyo wa KKKT na
kusisitiza kuwa, jambo ambalo halitakiwi litokee nchini.
Askofu
Malasusa alitoa wito kwa serikali kushirikiana na taasisi za dini
kikamilifu kudumisha umoja, amani na mshikamano wa kindugu miongoni mwa
Watanzania.
“Tumeshuhudia
uchomaji wa makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu,
Tunduru, Rufiji, Kigoma na hapa Dar es Salaam, vitendo ambavyo si
utamaduni wa Watanzania ambako kwa asili ni wamoja, wanapendana sana
wanashirikiana bila kujali tofauti ya dini zao,” alisema Malasusa na
kuongeza;
“Watanzania wengi wanasikitishwa sana vikundi vinavyochochea chuki na uhasama baina yao, hivyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi vinginevyo amani ya nchi yetu itakuwa mashakani.”Malasusa ambaye alisema kuwa, ingawa Tanzania inatajwa kuwa kisiwa cha amani, matukio yaliyotokea hivi karibuni yanatia shaka.

Alisema
kitendo cha kuchomwa moto makanisa na watu wanaodaiwa kuwa ni Waislamu
wenye msimamo mkali kilimuogopesha sana kwani lingeweza kutokea lolote
kama upande wa pili wangeamua kulipiza kisasi.
No comments:
Post a Comment