Bendi ya muziki ya dansi ya Sky Light ikitumbuiza katika sherehe za kutimiza miaka 20 ya Club Bilicanas na
miaka 13 ya Clouds FM.
Sherehe hizo zilipambwa na shamrashamra za aina mbalimabli ikiwemo kukati keki pamoja na kufungua shampeni
Dk. Lilian Mtei akizungumza katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Clouds FM, Wasiwasi Mwabulambo akizungumza katika hafla hiyo
Tukate keki
Mmoja
kati ya wafanyakazi wa kwanza wakati Bilicanas Club inaanzishwa miaka 20
iliyopita, Monika Victor akimlisha keki, Dk. Lilian Mtei wakati wa
hafla ya kutimiza miaka 20 ya klabu hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam usiku wa kuamkia leo.
Maandalizi ya keki
Pili
Mitemo ambaye alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu
hiyo, ambaye kwa sasa ni marehemu akipokea keki kutoka kwa Dk. Lilian
Mbowe kwa ajili ya kuwapa wadau waliojitokeza katika hafla hiyo
Mzee Ali Ramadhan Mkude nae akuwa mbali katika mnuso wa Bilicanas Club kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa
DJ Ibrahim Tuwa 'Dj Ibra' akilishwa keki wakati wa hafla hiyo
Dk.
Lilian Mtei akimlisha kipande cha keki Meneja Msaidizi wa Vinywaji wa
Club Bilicanas, Amandus Agant wakati wa Birthday ya Bilicanas Club
kutimiza miaka 20.
Monica Victor akigawa keki kwa wadau waliofika katika sherehe hizo.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa na mmiliki wa blog ya Bongoweekend, Khadija Kalili pamoja na wadau wengine.
Watu wa mataifa mbalimbali wakicheza muziki katika ukumbi wa Bilicanas.
WADAU
mbalimbali wa burudani usiku wa kuamkia jana walifurahia kwa pamoja
na kula keki ya miaka 20 ya klabu ya Kimataifa ya Bilicanas na miaka
13, ya Clouds Fm, iliyoambatana na shamrashamra mbalimbali ndani na
nje ya ukumbi huo.
Sherehe
hizo ziliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bilicanas Group, Dk. Lilian
Mtei ambapo aliwashukuru wadau hao kwa kuwa bega kwa bega na klabu
hiyo, tangu 1992. “Tunawashukuru sana kwa kuwa nanyi mara zote inatia
faraja kwetu na tutaendelea kutoa huduma bora siku zote|” alisema Mbowe.
Mtei pia
aliwashukuru wafanyakazi mbalimbali waliofanikisha ukumbi huo kufikia
hapo na kutoa heshima ya kipekee kwa wafanyakazi waliokuwapo tokea
inaanza hadi ilipofikia miaka 20 na hatimaye kukata keki hiyo.
“Uwepo wa
miaka 20, tuna kila sababu ya kuwapongeza wafanyakazi tuliokuwa nao
toka mwanzo hadi leo, na kwa heshima ya pekee Mama Victor na Mrs
Mitemo ndiyo watakao kata keki hii” alisema Mtei.
Keki hiyo
ilikatwa na wafanyakazi hao Monica Victor na Pili Mitemo ambaye
alimwakilisha mumewe aliyekuwa Meneja wa kwanza wa klabu hiyo, ambaye
kwa sasa ni marehemu.
Aidha,
kwa upande Clouds FM, iliwakilishwa na Wasiwasi Mwabulambo ambaye
alipongeza klabu Bilicanas kwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua sanaa
nchini hasa kwa kuwasaidia wasaidia wasanii kufikia malengo yao.
Kwa
upande wake Ibrahim Tuwa ‘Dj Ibra’ aliyekuwa akisherehesha shughuli
hiyo, aliwaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono na wataendelea na huduma
bora zaidi ha hapo. Dj Ibra alijiunga na Bilicanas tokea 2002,ambapo
mpaka sasa ana miaka 10 kwenye klabu hiyo iliyowahi kuwa na madj
maarufu waliopita hapo ambao wengi wao wapo kwenye vituo vya
televisheni na redio.
No comments:
Post a Comment