Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 4, 2012

Tundu Lissu kupambana na kaka yake kortini leo



RUFAA ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema kwa mara nyingine tena inatarajiwa kuwaweka katika mpambano mkali wa hoja za kisheria, Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu, na ndugu yake, Alute Mghway. 
Ndugu hao wanatarajiwa kupimana ubavu katika rufaa hiyo, inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la Majaji wa watatu wa Mahakama ya Rufani, linaloundwa na Jaji Salum Massati, Jaji Nathalia Kimaro na Jaji Bernard Luanda, kuanzia saa 3:00. Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ni mmoja wa mawakili wa mrufani (Lema), akisaidiana na Wakili Methods Kimomogolo.
Jaji Bernard Luanda aliyekuwa nafasi ya Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman
Akizungumza na Mwananchi jana, Lisu alithibitisha kuwepo mahakamani leo wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, tayari kwa mapambao ya hoja za kisheria, kumtetea Lema, akisaidiana na Wakili Method Kimomogoro.

Wakati Lisu akimtetea Lema, Mghway ni wakili anayewatetea warufaniwa (wajibu rufaa) ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel.


Makada hao walimfungulia Lema kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha wakipinga matokeo yaliyompa ushindi katika Uchaguzi Mkuun wa mwaka 2010 na kutokana na kesi hiyo, April 5, 2012, mahakama hiyo ilimvua wadhifa huo.

Kufuatia uamuzi huo, Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua ubunge, lakini rufaa yake ilitupiliwa mbali, baada ya mahakama kuridhika kuwa kulikuwa na dosari za kisheria, kufuatia pingamizi lililowekwa na warufaniwa.

Hata hivyo, tofauti na hoja za wakili wa warufaniwa, Mghway kuwa kutokana na dosari hiyo mrufani hana nafasi ya kufanya marekebisho, mahakama ilimpa Lema nafasi nyingine ya kufungua upya baada ya kusema kuwa dosari hizo zinarebishika.

Mahakama hiyo ilimpa Lema siku 14 kufanya marebisho na kufungua tena rufaa hiyo ndani ya muda huo. Tayari Lema ameshafungua upya rufaa baada ya kuifanyia marekebisho ya dosari zilizojitokeza na imepangwa kusikilizwa leo, huku kukiwa na mabadiliko ya jopo la majaji.

Awali rufaa hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Jopo lililoongozwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman akisaidiana na Jaji Salum Massati na Jaji Nathalia Kimaro, lakini kwa sasa Jaji Mkuu, Othman hayuko katika jopo hilo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji
Bernard Luanda.

Wakizungumzia usikilizwaji wa rufaa hiyo leo, mawakili wa pande zote wamesema kuwa wako tayari  Lema katika rufaa yake ya awali alitoa hoja 18 za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge, lakini tarehe ambayo rufaa hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa, wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughwai, aliweka pingamizi la awali.

Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake wa Novemba 8, 2012, kuhusiana na pingamizi hilo, licha ya kukubali kuwa kulikuwa na dosari za kisheria na kikanuni, ilimwamuru Lema afanye marekebisho ya dosari hizo na kuwalisha upya rufaa yake ndani ya siku 14.

Wajibu rufaa katika pingamizi lao walitoa hoja tatu za pingamiizi, wakidai kuwa kuna mkanganyiko katika ya vifungu vya sheria kati ya vile vilivyotunmika kwenye hukumu na vile vilivyokuwepo kwenye muhtasari wa hukumu (decree).

Hoja nyingine walidai kuwa muhtasari wa hukumu haukuwa na mhuri wa Jaji aliyeitoa wala tarehe na hoja ya tatu ilikuwa ni utaratibu wa kuandika muhtasari huo, kwa kutokuandika maneno, “imetolewa kwa mkono wangu na mhuri wa mahakama”.

Kutokana na hoja hizo, Wakili Mghwai aliiomba mahakama hiyo iitupile mbali rufaa hiyo, akidai kuwa kwa dosari hizo mrufani hana nafasi tena ya kuzifanyia
marekebisho.

Upande wa wajibu pingamizi, Wakili wa Lema, Kimomogoro, na Wakili wa Serikali Timoth Vitalisi kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wajibu hizo walidai kuwa kasoro zote zilizotajwa hazina athari na zinaweza kurekebishika.

Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali hoja mbili za rufaa kuwa hazina msingi na ikakubaliana na hoja moja ya pingamizi kwamba kulikuwa na tofauti au kuchanganywa kwa vifungu hivyo vya sheria.

Katika uamuzi wake wa Novemba 8, 2012, ilisema kuwa kisheria, hati ya muhtasari wa hukumu ni lazima ikubaliane na hukumu lakini katika shauri hilo
mushtasari wa hukumu ulikuwa haukubaliani na hukumu.

“Hukumu inarejea kifungu cha 114 (1)-(7), (Sheria ya Uchaguzi), lakini hati ya decree inarejea kifungu cha 113 (1)- (7).”, ilisema Mahakama hiyo na kuongeza:

“Decree lazima ikidhi masharti ya Amri ya XX, Kanuni ya 6 na 7, ZA Mwenendo wa Mashauri ya Madai, sura ya 33. Katika shauri hilI inakiuka Amri ya XX Kanuni ya 6 na 7, dosaria hiI inaifanya hati hiI isiwe halali.:

Hata hivyo mahakama ilisema kuwa inakubaliana na Mawakili wa wajibu pingamizi hilo kuwa kosa hilo linawezekana limetokana na kuteleza kwa kalamu ama kutokana na kosa la uchapaji.

“Kwa sababu hii linaweza kurekebishwa chini ya Kanuni ya 111 ya Kanuni za Mahakama.”, ilisema Mahakama na kumpa Lema siku 14 kufanya marekebisho ya dosari hizo na kufungua tena rufaa hiyo ndani ya muda huo.
You might also like:

No comments:

Post a Comment