Pages

Thursday, January 17, 2013

FIGO ZA DCI ROBERT KANUMBA HAZIFANYI KAZI.



MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania,Robert Manumba amezidiwa kiasi cha kupumua kwa msaada wa mashine katika Hospitali ya Aga Khan. 

Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.

Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.

Manumba amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututuzi (ICU) kwa ajili ya uangalizi wa jopo la madaktari,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilizoifikia BLOG HII zinadai kwamba Mkurugenzi huyo wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amezidiwa kiasi cha kupumua kwa kutumia mashine ya hewa safi ya Oxgen.

Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.

“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo. Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga Khan.

“Ni kweli amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendelea vizuri,” alisema Senso.

Mtu wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya malaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi. 

Daktari Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema jana kwamba Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo tangu juzi akisumbuliwa na malaria na alikuwa hajitambui.

“Nimepigiwa simu nyingi leo (jana), nikiulizwa na watu mbalimbali wakitaka kufahamu kama Manumba amefariki dunia, ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzima lakini yuko mahututi ICU"alisema Dk Dharsee.

No comments:

Post a Comment