Pages

Sunday, January 27, 2013

HALI NI MBAYA MTWARA DAMU YA WATU SABA YAMWAGIKA NYUMBA ZA WABUNGE ZACHOMWA MOTO


Nyumba  za  wabunge zikiteketea kwa moto
watuhumiwa wa vurugu wakikamatwa
nyumba  za wabunge  zilizochomwa  moto leo

Na Abdulaziz Video Lindi

WATU  saba akiwemo askari  polisi mmoja  wameuwawa huku  wengine  wakijeruhiwa  vibara katika vurugu  kubwa  zilizoibuka Mtwara mkoani Lindi leo


mbali ya watu hao  kuuwawa  pia Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa yaMtwara/Mikindani  yakoswa koswa kuchomwa moto  hii leo kwa kilekinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogocha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara


Vurugu hizo zilizoanza leo  zimehamia wilayani Masasi mkoani

Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi
Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha
ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku  Nyumba ya Mbunge wa Masasi(Mama
Kasembe),Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri
nayo yateketezwa kwa Moto mchana hii leo katika vurugu za waandamanaji
zilizoanza kwa waendesha Bodaboda kuanza kuandamana POLISI wakizidiwa
na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto ,

Taarifa za ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa

kufuatia simu za mkonononi za viongozi wa polisi kutopokelewa  ni
kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo
Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea
huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba
ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi

Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa

kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es
Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili  Mtwara leo
asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.

Maandamano hayo ya Vurugu yalioongozwa na Madereva wa boda boda.

Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari
nyumba moja imechomwa moto na baadhi ya magari huku Vijana wakizidi
kusonga mbel
e

No comments:

Post a Comment