Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akisalimiana na
wanaCC, wa mkoa wa Tabora mara baada ya kuwasili katika kituo kikuu cha
treni ya Reli ya Kati cha Tabora mjini. Abdurahman Kinana anaongoza
wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya
maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayofanyika
kwenye uwaTanganyika Februari 3 mwaka huu.
Wananchi wa Kituo cha Treni Salanda wakifanya biashara ya nyama ya kuku iria mbalimbali wanaosafiri na treni ya Reli ya Kati.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Singida Mgana Msindai mara baada ya kutika kituo cha Salanda Manyoni
mkoani Singida ambapo wana CCM waliandaa mapokezi, kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Manyoni John Chiligati
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.
Asha Rose Migiro katikati akicheza ngoma na wana CCM wa Singida.
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye
akizungumza na wana CCM wa Saland Manyoni Mkoani Singida wakati wajumbe
wa Sekretarieti ya CCM walipopata mapokezi wakielekea mkoani Kigoma.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM
Abdurahman Kinana ili kuongea na Wana CCM wa mkoa wa Singida kushoto ni
Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akiwasalimia wana CCM wa Mkoa wa Singida
katika kijiji cha Salanda Manyoni Mkoani Singida leo.
No comments:
Post a Comment