Kofia
ngumu za kusaidia kuokoa kichwa dhidi ya majanga mbalimbali iwe ni
katika maeneo ya ujenzi au katika vyombo vya usafiri ni muhimu sana
kwetu tunapokuwa katika mazingira hayo.
Tunaishukuru
serikali kwa kutumia idara zake husika kuhimiza matumizi ya kofia hizi
hasa kwa madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.
Kama
inavyojulikana mtu ni afya na pia tunafahamu kuna baadhi ya magonjwa ya
kuambukiza kwa njia ya kugusana, kutumia kitu kimoja watu wawili au
zaidi na mengine kwa njia ya maji, hewa, mbu, kujamiiana na kadhalika.
Hapa
kwenye hili la kofia ngumu bado hainiingii akilini vizuri jinsi gani
twaweza kukwepa magonjwa ya ngozi na mba japo sio lazima tuyapate wala
hatuyaombei ila tunaangalia uhalisia wa matumizi ya kofia hizi.
Ndugu
zangu wataalamu wa magonjwa ya ngozi na tiba hili likoje katika
uhalisia wake? Sichokonoi ila naomba kufahamu tu kwamba tuwe tunazifua?
Au hakuna neno? Mzingatie pia je zitakauka?.
Wadau sijasema msivae helmet la hasha nimeulizia tu ili woote tupate fahamu.
No comments:
Post a Comment