Pages

Saturday, January 26, 2013

TASWIRA ZAIDI YA VURUGU KATIKA MJI MDOGO WA DUMILA, WANANCHI WAKIMSHINIKIZA MKUU WA MKOA MORO KUSIKILIZA KILIO CHAO CHA KUNYANYASWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA WILAYA YA KILOSA.



Sehemu ya vijana wakiwa katika picha tatu tofauti mara baada ya kuchoma moto na kufunga barabara  barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa kuweka vizuwizi mbalimbali hali iliyopelekea watumia wa barabara hiyo kushindwa kuitumia kwa masaa matano kabla ya polisi kutuliza hali hiyo iliyoanza majira ya saa 2 asubuhi na kudumu hadi majira ya saa 7 mchana katika mji mdogo wa Dumila wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. 
 Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za wakulima.
 
 Askari wa kutuliza ghasia (FFU) Morogoro wakiangalia gari mara baada ya kuharibiwa wakati wa vurugu hizo kabla ya kulinyanyua.
Hapa askari na baadhi ya raia wakiwasaidia kuinyanyua gari hili 
 Gari hili likionekana mara baada ya kuharibiwa likiwa katikati ya barabara kabla ya kusukumwa na kulirejesha sehemu ambayo iliegeshwa.
 Mwananchi akizngumza jambo na askari wa kuliza ghasia muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kuhutubia wananchi hao na amani kurejea katika hali yake ya kawaida.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani kushoto akiawaangalia vijana waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili awahutubie.
Rasta Man kushoto akijaribu kuwatuliza wananchi wenzake kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhutubia. 
 Sehemu ya akinamama wakionyesha kukerwa na jambo wakati wa vurugu hizo, hapa walukuwa wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili kuweza kusikiliza kero zao. 
 Mmoja wa vijana akiwa na kreti ya soda mara baada ya kupora katika vurugu hizo.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akiwahutubia umati wa wananchi wa vijijini vyenye migogoro ya ardhi katika tarafa ya Magole wilaya ya Kilosakwenye uwanja wa shule ya msingi Dumila jana.
  Gari la mkoa wa Morogoro likiondoa eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la shule ya msingi Dumila wilaya ya Kilosa mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment