Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake, wakikaribishwa na
viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma baada ya treni kutoka Dar es Salaam,
kuwasili leo asubuhi mjini Kigoma, Wanaoshuka ni Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi
na Uenezi Nape Nnauye. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi
Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM
zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma. (Picha na Bashir
Nkoromo).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro (kushoto) wakisindikizwa baada ya kushuka kwenye treni mjini
Kigoma, ambako waliwasili leo wasubuhi wakitoka jijini Dar es
Salaam.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili
ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika
Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Mamia
ya wananchi wakiwa wamejitokeza kupokea msafara wa Kinana ulipowasili
kwa treni Stesheni ya Kigoma leo asubuhi. Kinana na ujumbe wake
wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha
maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini
Kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma kwenye stesheni ya
Kigoma, alipaowasili kwenye stesheni hiyo na ujumbe wake akitokea jijini
Dar es Salaam. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Walid
Kaborou na kulia ni Nape akishiriki kupiga ngoma.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru dereva wa treni Kambi Ali,
baada ya treni ya abiria aliyoendesha akiwemo Kinana na ujumbe wake
kuwasili mjini Kigoma leo asubuhi. Wengine Wapili kushoto ni Dk. Asha
Rose Migiro na Nape Nnauye
Kinana
akisalimiana na wananchi kwenye stesheni ya Kazuramimba leo saa 12,
asubuhi. ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma
kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM
zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimfurahia mtoto Ali Saidi
mwenye umri wa miezi minane, ambaye ni mtoto wa mmoja wa abiria
aliowakuta kwenye Stesheni ya Kigoma, msafara wa Kinana ulipowasili leo
kwa treni.
Mwananchi wa Kaliua akipeleka kupakia mchele kwenye behewa, treni ilipofika stesheni ya eneo hilo mkoani Kigoma leo.
Abiria kutoka Tabora kwenda Kigoma wakiwa katika behewa leo.
Kinamama
wa Uvinza, wakipeleka kuuza chumvi kwa abiria, treni ilipofika kwenye
stesheni ya eneo hilo la Uvinza leo ikitoka Dar es salaam kwenda Kigoma
No comments:
Post a Comment