Pages

Thursday, January 10, 2013

SIMBA NA AZAM KATIKA PICHA UWANJA WA AMAAN


Mgeni rasmi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akisalimiana na kiungo wa Simba SC, Jonas katika mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.

Mgeni rasmi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akisalimiana na kipa wa Azam FC, Mwadini Ally katika mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.

Kikosi cha Simba leo

Kikosi cha Azam leo

Kipre Balou wa Azam kulia akiwania mpira wa juu na Abdallah Seseme wa Simba

Samir Hajji Nuhu wa Azam akiwatoka wachezaji wa Simba

Miraj Adam wa Simba akiuwahi mpira dhidi ya Hajji Nuhu wa Azam

Humphrey Mieno wa Azam aliyeenda hewani kuifungia bao la kwanza timu yake 

Wachezaji wa Azam, Ibrahim Mwaipopo kushoto na Uhuru Suleiman kulia wakimdhibiti kiungo wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' katikati huku kocha wake Jamhuri Kihwelo 'Julio' kulia kabisa akishuhudia

Wachezaji wa Azam wakimpongeza Humphrey Mieno kufunga bao la kwanza

Paul Ngalema wa Simba akimdhibiti Uhuru Suleiman wa Azam FC

Ibrahim Mwaipopo anatoa pasi huku akiwa amebanwa na wachezaji wa Simba SC

Kipa wa Simba SC, William Mweta akiwa amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam, Brian Umony huku beki wake Paul Ngalema akiwa tayari kutoa msaada kulia

Seif Abdallah wa Azam akiwatoka mabeki wa Simba

Ramadhani Mkipalamoto akiwatoka mabeki wa Azam

Kipre Balou akimiliki mpira mbele ya Jonas Mkude wa Simba

Haruna Chanongo akitoa pasi kwa kichwa mbele ya Ibrahim Mwaipopo

Miraj Madenge wa Simba, akimiliki mpira mbele ya Himid Mao wa Azam

Himid ameosha mbele ya Madenge

Madenge akimpongeza Rashid Ismail kufunga bao la kwanza la Simba SC

Mwadini Ally amedaka mbele ya beki wake Himi Mao, huku Ramadhani Mkipalamoto akifukuzia

David Mwantika wa Azam akimdhibiti Mkipalamoto wa Simba SC

Samih Hajji Nuhu amempitia Mkipalamoto na mpira wake 

Daktari wa Simba SC akimtoa nje beki Hassan Hatibu baada ya kuumia kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo

Mkipalamoto amemlamba chenga Himid Mao, anaondoka...

Lakini shuti lake lilidakwa na Mwadini...lilikuwa bao la wazi sana alikosa

Gaudence Mwaikimba akipiga mpira kichwa ambao ulitoka nje sentimita chache 

Hatari langoni mwa Simba SC

Lakini salama...

Himid Mao akiwa ametoa mpira nje kupunguza kasi ya Haruna Chanongo wa Simba SC

Mwantika amezuia, anaanza kugeuka taratibu

Miraj Madenge akishangilia baada ya kuifungia Simba bao la pili

Kutoka kulia ni Hassan Khatibu na Rashid Ismail wakicheza na Miraj Madenge kumpongeza kwa kufunga bao la pili 

Mkipalamoto akitafuta mbinu za kumtoka Mwantika

Hapa ni wakati Azam ikiwa nyuma kwa 2-1, tazama sura ya kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall ilivyokuwa

Brian Umony akiwa benchi baada ya kutolewa 

Kipa wa Simba SC, William Mweta akigagaa mpira ukiwa nyavuni...ni baada ya mkwaju wa penalti wa Joackins Atudo kuipatia Azam bao la kusawazisha

Wachezaji wa Azam Seif Abdallah kulia na Humphrey Mieno kushoto wakiwa kwenye benchi baada ya kutolewa

Makocha wanne wa kigeni wa Azam wakiwapa mawaidha wachezaji wao kabla ya kuingia kumalizia dakika 30 za nyongeza

Kuna wakati ilibidi Stewart Hall aombe ushauri kwa mchezaji wake wa akiba, Luckson Kakolaki kushoto ambaye anamuambia cha kufanya, bila shaka ilikuwa ushauri mzuri na ndiyo maana timu ilishinda

Shujaa wa Azam, Malikqa Ndeule akiwa amebebwa juu juu  SOURCE  http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment