Pages

Wednesday, January 23, 2013

WIMBI LA UPORAJI LAIBUKA KITUO CHA MABASI UBUNGO KUTOKANA NA KUKATWA KWA UMEME


terminal
 KITUO cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani (UBT), kinakabiliwa na vitendo vya uhalifu, kutokana na sehemu kubwa kukosa umeme iliyosababishwa na bomoabomoa ya kukihamishia Mbezi Luis.Wakizungumza na Fullshangwe abiria na waangalizi wa mbasi kituoni hapo, walisema unapofika usiku hali inakuwa ya kutisha kutokana na giza totoro ambalo linawashawishi vibaka kuvamia eneo hilo.
 
Walisema miongoni mwa uhalifu unaofanywa na vibaka hao, ni kuibiwa mafuta kwenye mbasi, vyuma vya majengo yaliovunjwa na kuporwa abiria wanaofika usiku.
 
 
Alisema kabla kituo hakijavunjwa kila mfanyabiashara alikuwa na mlinzi wake, hivi sasa eneo hilo liko wazi kitendo kinachosababisha wezi kuongezeka.
 
“Usiku mnatisha unajua magari yenyewe yanatisha yanapokuwa mengi, hakuna mwanga kitendo kinchochochea wezi kupata maeneo ya kujifisha na kufanya vitendo vya uhalifu”alisema mmoja wa waangalizi wa magari hayo.
 
Naye James John, alisema kwa sasa kituo chote hakina umeme ukiondoa, jingo la polisi hali ambayo inasababisha huduma zote usiku kuwa duni hata ile sehemu ya kupunzikia wasafiri na vyoo ambavyo ni muhimu kwa wasafiri, ambako nako kuna giza.
 
“Tabu inakuwa alfajiri pale wasafiri wanapofika kituoni hapo, kwani inatuwia vigumu kubaini haraka magari tunayosafiri nayo kutokana na giza”alisema John.
 
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ili kutoa ufafanuzi, ilielezwa kuwa yuko safarini nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment