Kikosi
cha Young Africans Sports Club kimeendelea na mazoezi yake leo katika
uwanja wa Fame Residece Football uliopo Antalya kisha jioni timu ikaenda
kufanya mazoezi katika ufukwe wa bahari, eneo lililopo nyuma ya hoteli
Fame Residence ikiwa ni siku ya tatu katika ziara ya mafunzo nchini
Uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom.
Kocha
Mkuu wa klabu ya Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahishwa na
maendeleo ya kambi, kwani toka wameanza mazoezi jumatatu leo ni siku ya
tatu wakiwa nchini Uturuki na anaona mabadiliko makubwa kwa wachezaji
wake, huku akisema hofu iliyokuwepo kwa watanzania juu ya hali hewa ya
baridi kali si kweli kwani hali ya hewa katika mjii huu ni baridi kiasi
tu na hata leo katika mazoezi ya asubuhi palikuwa na jua.
Wachezaji
wanaendelea kuzoea mazingira, na kujifunza mambo mengi yanayohusu soka
kwani wageni mbalimbali waliofika katika mji huu wamekuwa wakipenda
kujua mengi kuhusiana na timu ya Young Africans na soka la Tanzania kwa
ujumla.
Majira ya
saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki timu ilifanya mazoezi
ya ufukweni katika ufukwle wa Hotelu ya Fame Residence pemebezoni mwa
Bahari ya Mediteranian.
Kocha wa
makipa wa timu ya Bayern Leverkusen jioni alishuhudia Young Africans
ikifanya mazoezi ya ufukweni ambapo alisema amefurahia kuifahamu timu ya
Yanga na wachezaji wake wanaonekana kuwa na morali ya kucheza soka,
hivyo anaamin ziara hii itaisaidia timu kuwa pamoja na kujiandaa vyema
na ligi alisema
Wakati
huo huo mchezaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna
Niyonzima amewasili jioni hii kuungana na wenzake kufuatia kuchelewa
kuunganisha ndege siku ya jumamosi usiku akitokea nchini Rwanda
alipokuwa amekwenda kuchezea timu yake ya Taifa.
No comments:
Post a Comment