ZITTO KABWE.
SPIKA wa
Bunge, Anne Makinda ametangaza mabadiliko ya Kamati za Kudumu za Bunge,
huku Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa
na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ikifutwa.
Kutokana
na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitaendelea kufanywa na Kamati
ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo itaendelea na jukumu lake la msingi
la kuchambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) na kwa Serikaki Kuu.
Kamati nyingine iliyofutwa ni ya sheria ndogo, huku Spika akiunda kamati mpya tatu na nyingine kuzifanyia marekebisho kadhaa ikiwa ni hatua ya kuimarisha usimamizi wa Bunge kwa shughuli za Serikali.
Akitangaza mabadiliko hayo muda mfupi kabla ya kuahirisha mkutano wa kumi jana, Makinda alizitaja kamati mpya kuwa ni Kamati ya Bajeti, Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, ambayo imetenganishwa kutoka Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
No comments:
Post a Comment