INAKISIWA kuwa katika kila dakika moja, watoto wa kike 19 wenye umri chini ya miaka 18 wanaolewa kwa nguvu duniani.
Kuwa
mtoto wa kike katika nchi zinazoendelea katika Bara la Asia (asilimia
46) na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (asilimia 38) ni mbaya zaidi
kutokana na kukithiri kwa ndoa za mapema na za kulazimishwa.
Kwa
mujibu wa shirika la kimaitaifa la kuchangia maendeleo ya watoto (PLAN)
wasichana zaidi ya millioni 14 wanaolewa wakiwa na umri chini ya miaka
18 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Nchi za Chad, Niger, na
Mali zinaongoza!.
No comments:
Post a Comment