Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 3, 2013

Mbunge wa Arusha Mjini Lema-CHADEMA amekabidhiwa Kiwanja cha kujenga hospitali ya Mama na Mtoto



CHADEMA ikiongozwa na kamanda Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa wamekabidhiwa kiwanja cha ekari 3 cha kujenga hospitali ya Mama na Mtoto. Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyowa kuwaahidi wananchi wa Arusha katika uchaguzi wa 2010. Kiwanja hicho chenye thamani ya dolla za kimarekanai USD300,000 sawa na Tsh 480,000,000/ kimekabidhiwa na kampuni ya Mawala Advocates waliowakilishwa na moja ya mawakili na wakurugenzi wa kampuni hiyo. Hatua hii inamaliza propaganda na uvumi wa shutuma zilizokuwa zikienezwa na mawakala wa CCM dhidi ya Lema kuwa amekabidhiwa kiwanja hicho na ameandikisha kwa jina la mke wake.

No comments:

Post a Comment