Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya
CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya
kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa sherehe
kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Chama
cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake
ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana
kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali
mkoani Humo.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maandamano hayo wakimshangilia Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiongea nao.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na
viongozi wengine wa chama wakijiandaa tayari kwa kuanza matembezi ya
mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi
wengine wa chama katika matembezi ya mshikamano yaliyofanyika leo mjini
Kigoma asubuhi.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza
jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kulia ni
Katibu wa Halmashauri kuu Oganizesheni Mohamed Seif Khatib.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose
Migiro akisalimiana na Dk. Rajab Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose
Migiro akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Kobondo Ndugu Venance Mwamoto,
Katikati ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganizesheni.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa
CCM Bara Mzee Philip Mangula, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu
Mwigulu Nchemba.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa
CCM Bara kabla ya kuanza kwa maandamano hayo leo asubuhi.
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza barabarani wakati maandamano hayo yakipita kuelekea Ofisi za CCM Mkoa wa Kigoma.
Kutoka
Kulia ni Dk. Rajab Rutengwe Kanali Fabian Masawe Mkuu wa mkoa wa Kagera
na mdau Alice wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maandamano hayo.
source full shangwe
No comments:
Post a Comment