Machangudoa
nchini Nigeria wamesema wamefurahia sana ushindi wa Super Eagles dhidi
ya Ethiopia katika mashindano ya AFCON yanayoendelea nchini Afrika ya
Kusini.
Machangudoa hao
kupitia chama chao cha aegis of Nigeria Association of Prostitutes
wamewasisitiza wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria kujitahidi na
kushinda kombe hilo. Katika taarifa iliyotolewa na kusainiwa na katibu
mkuu wa chama hicho Jessica Elvis.
“Tunapenda
kuwapongeza wachezaji na makocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Super
Eagles kwa kufuzu kuingia robo fainali raundi inayofuatia ya mashindano.
Tungependa kuwapa uhakika wa sapoti yetu ili waweze kuleta ushindi
nyumbani.
"Katika
kuonyesha sapoti yetu kwa timu ya taifa, tutatoa ofa ya wiki moja ya
mapenzi bure kwa Super Eagles ikiwa watashinda ubingwa wa Afrika,"
alisema katibu mkuu wa chama hicho cha machagundoa.
Inasemekana baadhi ya wanachama wa chama hicho wapo nchini South Africa wakiisapoti timu hiyo kwenye mashindano ya AFCON.
No comments:
Post a Comment