Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 20, 2013

INASIKITISHA::HUYU NDIO KIJANA ALIYEMUUA MAMA YAKE MZAZI KWA KUMKATA SHOKA

 




Frank Hillary, 27, aliyetambuliwa kuwa mlokole, amethubutu na kuweza kukatisha maisha ya mama yake, Ndolukasi Lugamo, 50, akitumia shoka kuondoa uhai wa mzazi wake.
KWELI kuelekea mwisho wa dunia, mengi yataonekana. Mtu unawezaje kumpiga shoka mama yako mzazi, aliyekutunza tumboni mwake kwa miezi tisa, akakunyonyesha, kukusomesha hadi kukua na kujitegemea?


Tukio zima, lilichukua nafasi Alhamisi iliyopita, Mtaa wa Malipula, Kata ya Chamwino, mkoani Morogoro na inadaiwa kwamba kabla ya mauaji, Hillary alimpiga vibao, mitama na mateke mama yake.



Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Pili Athuman, alidai kwamba siku ya tukio, kulitokea mabishano kati ya Hillary na mama yake.

“Yalikuwa mabishano kidogo lakini ghafla yule kijana alimvamia mama yake na kuanza kumpiga,” alisema Pili na kuongeza:
“Yule kijana ni mtoto wa pekee wa yule mama. Tunashindwa kuelewa mpaka sasa chanzo cha tukio hilo. Halafu wale watu ni walokole kabisa na siku zote walikuwa wanaishi kwa upendo.”

No comments:

Post a Comment