Mfanyabiashara wa Mbeya ambae ndie alikuwa dereva wa gari namba T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa msafara wa Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam hivi karibuni , akifikishwa mahakama ya Mwanzo Bomani Iringa jana kwa tuhuma za kujipatia gari aina ya fuso yenye tmanani ya Tsh milioni 30 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa mwanamke Venannsia Sanga wa Iringa (Picha na Francis Godwin)
Na Francis Godwin, Iringa
MFANYABIASHARA
mkazi wa Mbeya ambae alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili
T.328 BML aina ya Land Lover Discovery na kusababisha kifo cha askari
mwenye namba WP 2492 Coplo Elikiza Nnko wakati wa msafara wa Rais Jakaya
Kikwete jijini Dar es Salaam ,amefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama
ya Mwanzo Bomani mjini Iringa kwa tuhuma za kujipatia gari lenye thamani
ya Tsh milioni 30 .
Akisoma
shtaka hilo hakimu wa mahakamani hiyo ya Mwanzo Bomani Mheshimiwa Alois
Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 4
mwaka 2012 katika eneo la Miyomboni mjini Iringa .
Masua alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kutenda kosa hilo alitoweka na kujificha katika mikoa mbali mbali hapa nchini .
Hata
hivyo alisema kuwa mlalamikaji katika shtaka hilo baada ya jitihada za
kumtafuta kushindikana ndipo alipofika mahakamani Februari 15 mwaka huu
kufungua kesi namba 61 /2013 kuhusiana na mtuhumiwa huyo.
Alisema
kuwa kutokana na kufunguiliwa kwa kesi hiyo jeshi la polisi kwa
kushirikiana na mlalamikaji waliendelea kumsaka mtuhumiwa huyo bila
mafanikio na baada ya kutokea ajali iliyosababisha kifo cha askari huyo
wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam katika msafara wa Rais
Kikwete ndipo mtuhumiwa huyo alipokamatwa baada ya picha yake kuonekana
katika vyombo vya habari .
Mtuhumiwa
huyo amekana kosa hilo ambapo mahakama hiyo imesema kuwa dhamana yake
ipo wazi na kuwa mdhamini anapaswa kusaini hati ya dhamana ya yenye
thamani ya Tsh. milioni 15 masharti ambayo yalitimizwa na wadhamini na
mfanyabiashara huyo kutolewa kwa dhamana hadi Aprili 25 kesi hiyo
itakapotajwa tena.
Wakati
huo huo ndugu wa mfanyabiashara huyo walionyesha kuwazuia wanahabari
kumpiga picha wala kuandika habari hiyo kwa madai kuwa ni habari ndogo
ambayo jamii haipaswi kuijua na kumtaka mfanyabiashara huyo kujifungika
sura yake na kuondoka na msafara wa magari mawili ya kifahari katika
mahakamani hiyo
No comments:
Post a Comment