Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini iliwaona wana kesi ya kujibu katika
mashtaka yote matano yanayowakabili. Katika moja ya mashtaka hayo,
Sheikh Ponda na wenzake anadaiwa kula njama na wizi wa mali yenye
thamani ya Sh59.6 milioni.
Awali, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa alitoa uamuzi kuwa kina Sheikh Ponda wana kesi ya kujibu baada ya kupitia
Kesi
hiyo iliposikilizwa mara ya mwisho, Hakimu Nongwa alisema kuwa baada ya
Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kubadilisha ardhi ya ekari nne
iliyopo Chang’ombe Markazi na ekari 40 za Kampuni ya Agritanza Ltd
zilizopo Kisarawe, kuna baadhi ya Waislamu hawakuridhika.
Mbali
na mashtaka hayo, Ponda na mshitakiwa mwingine Sheikh Mukadam Abdallah
Swalehe wanakabiliwa na shtaka la uchochezi wakidaiwa kuwa kati ya
Oktoba 12 na 16, mwaka jana katika eneo la Chang’ombe Markazi, wakiwa
viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, waliwashawishi
wafuasi wao kutenda makosa hayo.
No comments:
Post a Comment