Pages

Thursday, April 25, 2013

HII HABARI YA UONGO MTUPU:::GODBLESS LEMA AHUSISHWA NA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA



MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameamuru polisi kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na wanafunzi walioshiriki kurusha mawe baada ya kutokea vurugu zilizotokana na kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Uhasibu Arusha, Henry Kago (22).
  
Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi jana alitangaza kufunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu zilizotokea chuoni hapo, ikiwemo ukiukwaji wa nidhamu na urushwaji wa mawe uliofanywa na wanafunzi hao kwa Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama.
  
Mulongo alitoa amri hiyo baada ya Lema kudaiwa kuingia chuoni hapo jana asubuhi na kufanya siasa bila kufuata utaratibu.
  
“Si jambo jema kwa Mbunge kuingia chuoni na kuhamasisha siasa kwenye jambo hilo la kifo badala ya kuwatuliza wanafunzi ili tujue kiini cha tatizo hili," alisema mkuu wa mkoa na kushutumu kwamba jambo hilo linabadilika badala ya msiba linawekwa chuki za siasa na wanafunzi nao kuingia kwenye mkumbo.
  
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, upo utata wa kifo cha Kago kutokana na wengine kudai ameuliwa na bodaboda eneo la Esami na Kanisa la Waadventista Wasabato karibu na chuo huku wengine wakidai alitoka eneo la Bugaluu.
  
Alisema polisi inachunguza utata wa kifo hicho cha mwanafunzi huyo aliyekutwa na simu yake ya mkononi.
  
"Naagiza polisi kumkamata Lema popote alipo na wanafunzi wengine pamoja na wakili wake,” alisema Mkuu wa Mkoa bila kutaja jina la wakili.

Kwa  mujibu  pia wa  RADIO FIVE ya  jijini  Arusha, Mkuu  huyo  wa mkoa wa Arusha bwana Mulongo amenukuliwa kwa nyakati  tofauti tangu  jana  akitaja uwezekano wa Lema kusababisha kifo cha mwanafunzi ili apate nafasi ya kufanya siasa chuoni hapo.

Credit:  Habarileo  na Radio five 
Lema anahusika vipi na kifo cha Henry?wakati kauawa juzi usiku na Lema alikuja chuoni hapo akitaka kusaidia wanafunzi wanashida gani na nini tatizo lao,na Lema aliwasihi sana wanachuo hao kutofanya maandamano mpaka mkuu wa mkoa afike,Na mkuu wa mkoa alipopigiwa simu na kuambia kinachoendelea alisema yeye hajui chuo cha uhasibu kipo wapi,Ni kweli wewe mkuu wa mkoa hujui mkoa wako na maeneo yake?Kafika eneo la tukio hataki kuongea anasema siwezi kupanda hapo juu na kuongea na nyie mpka mic iwepo kawekewa mic bado anaongea pumba,Hivi sis kodi zetu si ndo mishara yao?sasa kwanini hawtaki kusikiliza watu wanaowahudumia?wanaamua kutumi nguvu?.Na pia nyie gazeti la Habari leo msiwe mnakurupuka kuandika habari kwa upande mmoja tu jaribuni kuangalia pande zote ilikuaje na nini chanzo,wewe wanachuo ni wajinga waanze tu kuzomea na kufanya vurugu?lazima kulikuwa kuna kitu nyuma ambamcho kiliwafanya waamue kufanya hivo.R.I.P HENRY KAGO

No comments:

Post a Comment