Pages

Wednesday, April 24, 2013

MAWAZIRI WATOROKA BUNGE..VITI VYABAKI WAZI





Tabia ya utoro bungeni imejirudia tena mwaka huu wakati Bunge likijadili Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Safari hii utoro huo unawahusisha mawaziri na siyo wabunge.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea Julai 22, mwaka jana wakati wa mjadala wa Bajeti wa Wizara hiyo kiasi cha kufanya moja ya vikao vyake kuahirishwa kutokana na utoro wa wabunge.

Kutokana na utoro huo, jana asubuhi, Mbunge wa Mwibara
(CCM), Kangi Lugola alilazimika kuomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job Ndugai ili aone haja ya kusimamisha mjadala wa Wizara ya Kilimo kutokana na idadi ndogo ya mawaziri waliokuwamo ukumbini.

Lugola alisema Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ni mtambuka kutokana na kuajiri zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania na kwamba kutokana na nchi kukabiliwa na tatizo la chakula hivi sasa, inapojadiliwa inahitaji umuhimu wa kipekee.

No comments:

Post a Comment