Pages

Monday, April 15, 2013

Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame afariki dunia




Picture
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

14 Aprili, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013  saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika Hosptali ya TMJ.


Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea nidhamu na uzalendo.
Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment