Pages

Saturday, April 13, 2013

MFANYA BIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AFARIKI KWA AJALI YA NDEGE,ALIPOKUWA ANATUA UWANJA WA NDEGE ARUSHA



-
 PICHA NA MAKTABA
 Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawalla aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi, imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha Arusha.
- Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama "Bob Sambeke" aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro ambaye naye kapoteza maisha (kafariki)!
- Inadaiwa kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja (saa 12.30 jioni) kupita.

BOB SAMBEKE ALIYEKUWA RUBANI WA MAREHEMU WAKILI MAWALA. NYAGA NAYE KAFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA.
MAANDISHI KWA HISANI YA JAMII FORUM

No comments:

Post a Comment