Pages

Sunday, April 14, 2013

MWANDISHI MAARUFU WA BLOG MJENGWA,AKAMATWA TUHUMA ZA KUSHAMBULIWA KWA KIBANDA.



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.Majid Mjengwa.
DAR ES SALAAM:  
MWANDISHI wa safu katika magazeti mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa Kibanda.

Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso aliliambia Mwananchi kwamba:

“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”

Hata hivyo, Senso hakuwa tayari kueleza kwa undani muda aliokamatwa Mjengwa wala sababu za kukamatwa na kuhojiwa kwake, lakini chanzo chetu ndani ya Jeshi la Polisi kilithibitisha kwamba pamoja na mambo mengine kuhojiwa kwake kulihusu uteswaji wa Kibanda.
SOURCE AUDIFACE BLOG

No comments:

Post a Comment