Pages

Monday, April 15, 2013

PICHA: Magari yaliyogongana mkoani GEITA na kusababisha kifo cha aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Makosa ya jinai,SSP MAGNUS BONIFACE MNG'ONG'O 13/04/2013 katika Kijiji cha Chibingo kata ya Nyamigota Barabara ya Geita – Chato.


Picha za Magari yaliyogongana mkoani GEITA na kusababisha kifo cha aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Makosa ya  jinai,SSP MAGNUS BONIFACE MNG'ONG'O 13/04/2013 majira ya saa20:30 HRS katika Kijiji cha Chibingo kata ya Nyamigota Barabara ya Geita – Chato.
Gari no T.467 ANG MITISUBISH FUSO,iliyokuwa ikiendeshwa na SAID KHALIFANI,MIAKA 38.Mkazi wa Mwanza,iligongana na Gari no.429 BMN TOYOTA COLLORA iliyokuwa ikiendeshwa na MAGNUS BONIFACE MNG'ONG'O mkuu wa upelelezi wa Geita.

Aidha mkuu wa upelelezi alikuwa kazini akitokea Wilaya ya Chato-Buselesele akielekea Geita mjini,akiwa njiani ndipo alipo pata ajali.


Alifariki wakati akipatiwa matibabu,katika hospitali ya wilaya ya Geita usiku,chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na katika ajali hiyo hakuna majeruhi,Hata hivyo dereva wa Fuso anashikiliwa kwa upelelezi.


Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa mazishi mkoani  IRINGA.



Taarifa yake Kaimu Kamanda wa polisi,
Kamishina Msaidizi wa polisi,
 JAPHET J.LUSINGU.

No comments:

Post a Comment