Rais Jakaya
Kikwete
---
Wizara
ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa
barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na
urefu wa kilomita 65.14. Aidha, sherehe hizo zitahudhuriwa na Bw. Daniel Wolde
Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa
Marekani.
Barabara ya Tanga –
Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Kenya
kupitia mkoa wa Tanga. Mradi huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia
Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation –
MCC).
Kukamilika kwa barabara hii
ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu
muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii kutapanua
fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri zaidi
fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Sherehe hizi zitafanyikia
kijiji cha Kisera katika Wilaya ya Nkinga mkoani
Tanga.
Taarifa hii imetolewa
na;
Balozi Herbert E.
Mrango
KATIBU
MKUU
No comments:
Post a Comment