Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye
tracksuti ya bluu),Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt.
Fenela Mukangala (wa tano kulia) na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh.
Christopher Ole Sendeka,wakishiriki katika matembezi ya nusu kilomita
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kufariki kwa Waziri
Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,yaliyofanyika leo huko
Kijijini kwao Monduli Juu,Mkoani Arusha.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka
shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward
Moringe Sokoine,aliefariki miaka 29 iliyopita siku kama ya leo.
Waziri wa
Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada
la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe
Sokoine.
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Mume wao.
Mbunge wa
Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri
Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine zilizofanyika kijijini
kwake Monduni Juu,Mkoani Arusha leo.
Baadhi ya
vijana wa jamii ya Kimasai wakikimbia mbio fupi za kumuenzi Waziri Mkuu
wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,kijijini kwake Monduli
Juu,Mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment