Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi,
Augustina Mmbando, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumain Kweka alidai kuwa
mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando
na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa mshtakiwa alifanya makosa hayo
kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu.
Kweka alidai kuwa Agosti 2, 2011 katika ofisi za
Mkemia Mkuu wa Serikali, akiwa mtumishi wa umma aliiba Sh40 milioni mali ya
Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira.Katika shtaka la pili, Kweka alidai kuwa Septemba 5,mwaka huo katika ofisi hizo aliiba Sh45 milioni mali ya Serikali zilizofika kwake kulingana na nafasi yake ya ajira
No comments:
Post a Comment