Pages

Saturday, April 20, 2013

WAMILIKI WA DALADALA: NAULI ZILIZOPANGWA NA SUMATRA BADO NI KIDUCHU KWAO!



d

WAKATI wananchi wakilalamika kupanda kwa nauli kuwa kumeongeza ugumu wa maisha, Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Daladala, Sabri Mabrouk amesema bado nauli hiyo ni kiduchu. Mabrouk aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, kuwa wananchi wanapaswa kutambuwa kuwa ugumu wa maisha haukuanza leo.

 Alisema hali hiyo haikusababishwa na kupanda kwa nauli bali ulikuwepo tangu utawala wa awamu ya kwanza na utaendelea kuwepo katika tawala mbalimbali zitakazokuja.

 “Kwa watu tulioishi katika maisha ya ugumu ugumu ni kisema hivyo wananielewa lakini najua wapo ambao wamenufaika kutokana na kuwa na jamaa ambao walikuwa viongozi katika serikali hao labda ndio wanaweza kushindwa kujua ugumu wa maisha katika nchi hii.

No comments:

Post a Comment