Mpambe
wa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, (mwenye nguo ya mabaka
meusi) aliyesimama nyuma ya kiongozi huyo, akiwa makini kuangalia
usalama wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya shule ya Msingi
Matarawe leo kuhusu vita dhidi ya mafisadi na umuhimu wa wananchi hao
kujiunga na Chadema. Chama hicho kimekamata kata tano nafasi za udiwani
Jimbo la Songea mjini zikiwa ni Kata ya majengo, Misufini, Mfaranyaki,
Bombambili, Lizaboni na Bombambili. Mkutano huo uliopigwa marufuku na
baadae kuruhusiwa kwa hekimas za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe Said Thabit
Mwambungu kutokana na kukubaliana na vingozi wa Chadema kutofanya
maandamano.Tendo hilo limewafanya chadema leo kumsifu mkuu wa mkoa huyo
hadharani kwa maauzi yake. (Picha na Maelezo yote na Juma Nyumayo) |
No comments:
Post a Comment