WAKATI
kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare
ikitarajiwa kusikilizwa lEo Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura (Lady
JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kesi hizo
zinatarajia kuvuta hisia za watanzania kutokana na mvuto na aina ya
kesi hizo,Lwakatale atapanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia
kupata dhamana ya kesi yake baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya
Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili awali na ambayo ilikuwa ikimnyika dhamana
na kubaki na shitaka la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo
inadhaminika.
Kwa upande wa
Lady JayDee anatarajia kupambanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya
kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho
mei 27 .Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo
pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari
zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio
Ruge Mutahaba.
No comments:
Post a Comment