Pages

Friday, May 3, 2013

GODBLESS LEMA: NIMEAGA FAMILIA YANGU




MBUNGE wa Arusha Mjini Godbless Lema, amesema tangu alipoamua kupigania haki za wananchi Mbunge wa Arusha Godbless Lema (kushoto), akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Arusha na vitongoji vyake katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro. Picha na Abraham Gwandu.
Arusha alikwisha itaarifu familia yake kuwa iwe tayari kupokea mwili wake akiwa amekufa. 
Lema alisema maneno hayo jana jioni katika viwanja vya shule ya Msingi Ngarenaro, wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha katika kile alichoita kutoa ufafanuzi wa tukio la yeye kuhusishwa na vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu wiki iliyopita." 
Familia yangu, inafahamu na nilishaiarifu, kwa sababu napigania haki za wananchi, wawe tayari kupokea maiti yangu na si mgonjwa mwenye majereha," alisema.
Mbunge huyo, alitumia muda mwingi kumshambulia kwa maneno makali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kama ndiye tatizo kubwa la demokrasia mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment