Pages

Monday, May 20, 2013

HUYU NI MTANGAZAJI WA NURU FM ALIYEKAMATWA NA KUCHEZEA KICHAPO KTK VURUGU ZA MACHINGA NA POLISI


 Watangazaji  wa Nuru  FM kutoka  kushoto Shadrack Mwansasu  na  Yusta  Msowoya  kulia  wakimpa pore  mtangazaji mwenzao Husein Farahan ambae leo alikamatwa na polisi wakati akielekea kazini na kuchezea  kipigo na kuwekwa  rumande
 Mwili  wa mtangazaji Husein Farahan  ukiwa  umevimba baada ya  kichapo kutoka kwa askari  wa FFU  leo
 Kichapo  kilikuwa kikali  kweli asimulia mtangazaji huyo

Mtangazaji  wa kituo cha Nuru FM Husein Farahan amesimulia kilichomkuta  kuwa  alikuwa katika usafiri na boda  boda na kusimamishwa na polisi kabla ya  kuchezea kipigo
Mtangazaji huyo alisema kuwa alikamatwa  eneo la Mshindo baada ya askari hao kumsimamisha na kuanza  kutembeza  kipigo na kuwa amepatwa na majeraha mgongoni kutokana na kupigwa  virungu mtindo mmoja.
Hata  hivyo kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema  kuwa  mbali ya mtangazaji huyo kukamatwa  pia wapo askari  polisi  waliokamatwa kutokana na kutofahamika na kuwa askari hao ni  wanachuo ambao  wapo mjini hapa kimasomo japo  kwa  sasa  wameachiwa  huru.
Kamuhanda amesema  kuwa  waliokamatwa  hadi saa 3 usiku  walikuwa ni  watu  zaidi ya  100 na  kuwa baadhi yao  wameachiwa na  wanaoendelea kushirikiliwa ni 80 na kesho leo  watafikishwa mahakamani .

No comments:

Post a Comment