Watangazaji
wa Nuru FM kutoka kushoto Shadrack Mwansasu na Yusta Msowoya
kulia wakimpa pore mtangazaji mwenzao Husein Farahan ambae leo
alikamatwa na polisi wakati akielekea kazini na kuchezea kipigo na
kuwekwa rumande
Kichapo kilikuwa kikali kweli asimulia mtangazaji huyo
Mtangazaji
wa kituo cha Nuru FM Husein Farahan amesimulia kilichomkuta kuwa
alikuwa katika usafiri na boda boda na kusimamishwa na polisi kabla ya
kuchezea kipigo
Mtangazaji
huyo alisema kuwa alikamatwa eneo la Mshindo baada ya askari hao
kumsimamisha na kuanza kutembeza kipigo na kuwa amepatwa na majeraha
mgongoni kutokana na kupigwa virungu mtindo mmoja.
Hata
hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema
kuwa mbali ya mtangazaji huyo kukamatwa pia wapo askari polisi
waliokamatwa kutokana na kutofahamika na kuwa askari hao ni wanachuo
ambao wapo mjini hapa kimasomo japo kwa sasa wameachiwa huru.
Kamuhanda
amesema kuwa waliokamatwa hadi saa 3 usiku walikuwa ni watu zaidi
ya 100 na kuwa baadhi yao wameachiwa na wanaoendelea kushirikiliwa
ni 80 na kesho leo watafikishwa mahakamani .
|
No comments:
Post a Comment