WAZIRI SAMUEL SITTA.
MWANZA.
WAZIRI wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema wakati ukifika,
yeye na rafiki zake Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe, watachagua mmoja wao watakayeona anafaa kuwania
urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Waziri
Sitta aliyasema hayo jana katika Kongamamo la Mawasiliano katika Nyanja
za Digitali la wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha
St. Augustine (SAUT), Mwanza.
Mara ya kwanza, Sitta aliwata
ja rafiki zake hao juzi wakati wa harambee ya kuchangia Kanisa Katoliki, Josephine Bakita, Parokia ya Igoma, Mwanza.
Pia
alisema hatagombea tena Ubunge Urambo ya Mashariki baada ya kuwa katika
ulingo wa siasa kwa miaka 35 na badala yake ataangalia namna nyingine ya
kuwatumikia wananchi huku akigusia mchakato wa kuwania urais ambao,
alisema anamwachia Mungu.
“Kwa
ubunge nimekwisha waeleza inatosha sitagombea tena kwani miaka 35
inatosha, … lakini hatima yangu ni nini siwezi kujua lakini nina afya
nzuri na mmoja wa wanasiasa wakongwe, wenye afya nzuri, mnaona
ninavyopendeza... kwa urais namwachia Mungu tutaona,” alisema Sitta.
Alisema
yeye rafiki zake hao wana mawazo yanayolingana katika mustakabali wa
nchi hii na kwamba wataendelea kutembea sehemu mbalimbali za nchi
kuwajengea wananchi uelewa ili wajue kuwa uongozi ni lazima ukae katika
mikono salama.
“Tutaendelea
kupita katika nchi hii kuwaeleza wananchi kujua uongozi wa nchi hii
lazima ukae katika mikono safi na ikitokea mmoja wetu akatamani urais,
basi tutaona inavyofaa, lakini tutasubiri watu wanavyosema pia kuhusiana
na nasi,” alisema.
Akijibu
swali la mwanafunzi wa SAUT kuhusiana na kumuunga mkono Rais Jakaya
Kikwete wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ilhali akijua kwamba hawezi
kuwaletea maisha bora wananchi, alisema kwake ilikuwa ni sawa na
kuchumbia na kwamba wakati wa uchumba, mchumba huonekana kuwa bora
lakini anaweza kubadilika wakati wa ndoa.
“Sikufanya
kosa kuwa katika mtandao wa Rais Kikwete, hii ni sawa na kuoa.
Unachumbia. Mchumba hawezi kuwa sawa wakati wa ndoa au wa kuwa mke,
inawezekana katika kugombea mtu akawa sawa lakini baadaye akajifunua
zaidi mambo yake, huwezi kumjua zaidi mtu labda uwe na Umungu,” alisema
Sitta na kusema: “Hata wapiga kura huwakuta hilo kwa kuchagua mtu ambaye
huenda kinyume na matarajio yao.”
Hata
hivyo, alisema kauli hiyo haina maana kwamba Rais Kikwete hakufanya
kitu, bali amefanya mambo mengi na kusema uzuri wa uongozi unapimika
wakati anapotoka madarakani hasa pale historia inapoandikwa na
kulinganishwa na marais wengine wajao na waliopita.
Katika kongamano hilo la SAUT, Waziri Sitta alifuatana na kada wa CCM, Paul Makonda.
No comments:
Post a Comment