Jumuiya
ya Wafanyabiashara wa Kariakoo wameahidi kuendelea kutafuta suluhu kwa
njia ya mazungumzo na serikali juu ya mgogoro wa makontena ambayo
yamezuiliwa bandarini, kitendo ambacho kimeathiri biashara zao kwa mda
mrefu sasa kwani wemeshindwa kufanya biashara ndani na nchi jirani kwa
takriban zaidi ya wiki tatu.
Tamko
hili lililotolewa na Jumuiya Hii wiki iliopita, limeeleza kuwa tayari
wametuma maombi kwa wizara husika na idara za serikali za mapato ili
kuwepo na mkutano utakaoweza kutizama jinsi ya kutatua mgogoro wa
makontena zaidi ya 400 ambayo yamezuiliwa bandarini.
Katika
tamko hilo imeelezwa kuhusu dhamira yao ya kukutana na Waziri wa Fedha
na Uchumi, Waziri wa Viwanda na Uwongozi wa TRA pamoja na vyombo vingine
husika ili kujadili na kutafuta ufumbuzi wa kile wanachodai ni ongezeko
la kodi.
Wanasisitiza kuwa kuwepo kwa pande zote hizi kwenye mkutano kutawezesha kufikia ufumbuzi.
Jambo
lililopelekea kufikia uamuzi huu wa kukutana na viongozi ni kile
walichokiita kutekwa nyara kwa kikao cha awali kilichofanyika na Waziri
wa Fedha ambapo Chama cha Mawakala wa bandarini kilifunika nafasi hiyo
kwa kujadili matatizo yao wenyewe bila ya kujali kero inayowakabili
wafanyabiashara ambao tayari wameanza kupata hasara kutokana na makotena
yao kukwama.
Wafanyabiashara
wamelalamika juu ya mawakala kuingia katika malumbano yao binafsi juu
ya ushindani wa kibiashara badala ya kutafuta suluhisho la makontena
yalio na bidhaa za wafanyabiashara hawa wadogo wadogo.
Hata
hivyo tamko la wafanyabiashara limeweka wazi kuridhika kwao na maelekezo
yaliyotelewa na Waziri wa Fedha na maafisa wa TRA juu ya kukubali kwao
kufanya kikao haraka na wafanyabiashara hawa.
Wafanyabiashara
pia wametakiwa kujaza fomu upya ambazo zitaeleza upya aina za bidhaa
walizoleta nchini na vielezo kamili vya bidhaa hizo ili vifanyiwe
uhakiki upya.
Pia
wamehakikishiwa kuwa hawatatozwa faini kwa makosa yoyote yatayobainika
baada ya kuhakiki fomu zao upya, iwapo zitakuwa na dosari.
Jumuiya
hiyo pia imesema kwamba iwapo kulikuwa na ukwepaji wa kodi basi badala
ya TRA kuwaadhibu wao nivema wangechukua hatua dhidi ya wale wote
waliokwenda kinyume.
Katika malalamiko yao wanadai kuwa ushuru wa forodha (Import duty) na VAT zimeongeka mara mbili bila ya wao kupewa taarifa.
Pia
wanadai kuwa TRA haikufuata utaratibu katika kuongeza kodi.Wanadai pia
wafanyabiashara wanalalamika juu ya HS Code ambayo inatumika kuonyesha
aina ya bidhaa mbali mbali na ushuru wake kwa madai ya kuwa
imechakachuliwa.
Lakini
wafanyabiashara wameendelea kusisitiza kuwa wao ni wananchi wenye kutii
sharia za nchi na wako tayari kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili katika
meza ya mazungumzo.
Wameelezea
jinsi walivyoanza kupoteza wateja wao mara baada ya mizigo yao
kuzuiliwa bandarini, ikiwa ni pamoja na usumbufu mkubwa kwa wateja wao
ambao wanatoka katika nchi za Afrika mashariki na nyinginezo.
Wamesema
hivi sasa kuna uwezekano wa wateja wao kuhama na kufanya biashara nchi
nyingine jambo ambalo litaipotezea taifa kiwango kikubwa cha pato la
taifa.
Wafanyabiashara
hao wanadai kuwa tayari wapo wenzao ambao wamekufa kutokana na
kutetereka kwa biashara zao baada ya kuambiwa walipe kodi kubwa ambayo
imewaletea mshituko mkubwa hadi kufikia kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na jumuiya, tayari mali ya mabilioni imekwama na gharama za kuukomboa zinaongezeka.
No comments:
Post a Comment