TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la
Polisi nchini linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa ambayo imekuwa
ikiripotiwa katika gazeti la Jamhuri la siku ya Jumanne tarehe 21 – 27
Mei, 2013 toleo No. 81 na la tarehe 28 Mei -Juni 3, 2013 toleo No. 83,
yenye kichwa cha habari "MTANDAO WA MAUAJI YA BARLOW WATAJWA NA IGP
MWEMA AMPA HIFADHI MUUAJI WA BARLOW"
Taarifa
hiyo siyo sahihi, kwa sababu mtu aliyehojiwa na gazeti hilo
anayejulikana kwa jina la Mohamed Edward Malele ni mgonjwa wa akili
ambaye mpaka hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
matibabu. Mara kadhaa mtu huyo amekuwa na tabia ya kuwatuhumu viongozi
na watu mbalimbali juu ya tuhuma zisizo na ukweli wowote kutokana na
ugonjwa wake wa akili.
Jeshi
la Polisi nchini linatoa rai kwa gazeti la Jamhuri kuwa makini na
habari wananzoziandika ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha zenye
lengo la kupotosha jamii.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment