Pages

Saturday, May 4, 2013

Ughaibuni si shwari ! Nani kachonga deal la kuibiwa kamanda Ras Makunja wa FFU ?



Watu wasio julikana wafanikiwa kuiba ndege wa Kamanda Ras Makunja !
Moja ya ndege wake amepatiaka katika kituo cha ifadhi ya wanyama !



Kamanda anamlaumu jirani kuwa ndie alichonga deal!

Na mpekuzi wa habari ughaibuni,

Habari za uhakika zimevuja kuwa mkuu wa bendi hisiyo kaukiwa na  virungu "Ngoma Africa band" aka FFU kule Ujerumani ,kamanda wao Ras Makunja amejikuta akishika kichwa baada ya watu wasio julikana kuingia katika imaya yake kuvunja moja ya matundu yaliokua na ndege aina bundi jirani ya nyumba 
na kutoweka nao ! inasemekana kamanda na familia yake walikua hawapo nyumbani,na wajanja awakatumia nafasi hiyo.

Kamanda Ras Makunja alishikwa na butwaa baada ya kugundua kuwa kwenye chumba kilichokua na ndege aina bundi mlango uko wazi na ndani hakuna ndege!

Baada ya kuenda kurepoti Polisi ikagundulika kuwa Bundi wawili wa kamanda walichukuliwa na idara ya kuifadhi wanya ya Ujerumani,kwa madai kuwa ndege hao walikua wakubwa mno na chumba chao ft 12X12 hakitoshi.
Kwa kupitia wakili wake mkuu wa kikosi kazi kamanda Ras Makunja ameambiwa bora awaruhusu ndege hao warudishe katika nchi za joto walikotoka,
Bundi hao walikua katika imaya ya mwanamuziki huyo kama ndege wa kufuga nyumbani,ambao alipewa na moja wa marafiki zake miaka ya nyuma.

Moja wa majirani wa kamanda Ras makunja ndiye anayetupiwa lawama na kamanda huyo kuwa awapendi ndege hao aina ya bundi, na jirani naye anarudisha
lawama kwa kudai labda baadhi ya wanafamilia ya kamamnda ndio waliotengeneza fitina ya kuondolewa kwa bundi hao,kwani walikuwa wanatisha.
Mwanamuziki kamanda ras Makunja anatafuta mbaya wake aliyesabisha kuchukuliwa kwa bundi wake ambao ana kibali cha kuwamiliki katika imaya yake ya Anunnaki Empire.
Tunampa pole kamanda ras makunja kwa yaliyomkuta.


No comments:

Post a Comment