Kamanda
wa Polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki akipanga maneno ya tembo
kulingana na uneno /uzito kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake.
Mwandishi wa habari wa katika Gazeti la Mtanzania Hamoni Mtega akiwa amenyanyua jino la tembo
————————————————–
JESHI
la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata meno ya Tembo 18 yenye
uzito wa kilo 84 yenye thamani ya Tsh216,000,000/ambapo meno hayo 18 ni
sawa na dola 15 elfu za kimarekani pia ni sawa na Tembo tisa waliouwawa
.
Akiongea
na waandishi wa habari ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani
Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamata meno hayo
lilitokea Juni 20 Mwaka huu majira ya saa 3.00 usiku katika kijiji cha
Majala kata ya Nandembo iliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma .
Kamanda
Nsimeki amesema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo
lilitokea baada ya askari polisi wa wilaya hiyo kupata taarifa kutoka
kwa wasamaria wema ndipo wao waliweka mtego wa kuwanasa watuhumiwa hao
lakini bahati mbaya watuhumiwa hao walikurupuka na kuacha mizigo ya meno
hayo iliyokuwa imefungwa kwenye mifuko tofauti tofauti.
Alisema
kuwa watuhumiwa waliokurupuka walikuwa wanne huku kila mmoja na
baiskeli ambazo walikuwa wamebebea meno hayo na kwa upande wa watuhumiwa
wa meno ya tembo kukurupuka bila kutiwa mbaroni na jeshi hilo limekuwa
ni tukio la pili la kwanza lilitokea katika kijiji cha Hanga wilayani
Namtumbo na la pili ndiyo hilo la wilaya ya Tunduru zote za mkoani
Ruvuma .
Aidha
kamanda alisema kuwa jeshi la polisi linajitahidi kuwasaka watu ambao
wamejificha na wanajihusha na matukio hayo ya ujangili kwa wanyama na
hasa tembo.
Pia
ametoa wito kwa wananchi uendelea kushirikiana jeshi la polisi mkoani
Ruvuma kwa kutoa taarifa za siri zitakazowezesha kukamatwa kwa wahusika
wa vitendo vya uhalifu wa aina yoyote kwa sababu suala la ulinzi ni kila
mmoja hivyo kunasoaswa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu baina ya polisi
na wananchi.
Picha na habari kwa hisani ya DemashonewsBlog
No comments:
Post a Comment