Social Icons

Featured Posts

Sunday, March 1, 2015

Izzo Bizness: Bado sijafikia uwezo wa kufanya video ya thamani ya milioni 40apper huyo ambaye wiki hii ameachia video na wimbo mpya uitwao ‘Kidawa’ aliomshirikisha Shaa, amedai kuwa nia ya kwenda kimataifa ipo na anajipanga kufika huko pia.
 “Natamani sana kufanya kazi nje ya nchi, kuna watu wametangulia wameenda na wameleta kazi nzuri tunaziona, lakini natamani na mimi nikienda nikirudi watu wasema ‘dah jamaa kwelia alienda,” Izzo alisema.

Wanaolala sana kushikwa na kiharusi

Mgonjwa anayeugua ugonjwa wa kiharusi

Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.
Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.

Kiongozi wa upinzani auawa Urusi


Maafisa wa polisi wakiweka usalama katika eneo ambalo kiongozi wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov aliuawa
Mmoja wa wanasiasa maarufu wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov ameuawa kwa kupigwa risasi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Moscow.
Mwanasiasa huyo alipigwa risasi nne kutoka nyuma na watu waliokuwa ndani ya gari alipokuwa akitembea nje ya makao makuu ya serikali.
Bwana Nemtsov ambaye alihudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa uongozi wa rais Boris Yeltsin alikuwa akimshutumu vikali rais Vladimir Putin.

Boris Nemtsov
Alikuwa akipanga mkutano ambao ungefanyika Leo

Mafuriko yawaua watu 14 MadagascarMafuriko nchini Madagascar yamewaua watu 14
Watu 14 wameuawa kwenye mafuriko nchini Madagascar ambapo pia wengine 20,000 wamelazimika kuhama makwao.
Mafuriko hayo yaliukumba mji mkuu Antananarivo na maeneo yaliyo karibu.
Utawala unasema kuwa mvua nyingi siku zijazo huenda ikasababisha madhara zaidi.

Saturday, February 28, 2015

BREAKING NEWSSS:::TIBAIJUKA,NGELEJA NA CHENGE WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA KAMATI KUU CCM,SOMA TAMKO ZIMA HAPAKAMATI KUU ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 28/8/2015, kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na moja alasiri, kimeazimia yafuatayo;

> Kamati Kuu imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, msanii wa Chama na Kada wa muda mrefu Mheshimiwa John Damian Komba.

Mwenyekiti wa CCM, Mhe Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa Chama hasa katika wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi na pengo ambalo ni vigumu kuliziba.

CCM imepata pigo na Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Kapteni John Damian Komba.

BREAKING NEWS!!! KAPTENI KOMBA AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Mbinga Magharibi na mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) Kapten John Komba amefariki dunia muda huu.
 Katibu mipango wa TOT, Gasper Tumaini 

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 28/02/2015

RATIBA YA MECHI ZA LIGI YA UINGEREZA ZITAKAZOCHEZWA LEO JUMAMOSI


NEW HIT SONG::::CHEKECHA CHEKETUA BY ALIKIBA DOWNLOAD NA SIKILIZA HAPANEW HIT VIDEO::JAGUAR MWAKA HUU ITAZAME HAPA