skip to main |
skip to sidebar
KAJALA AKUNUSHA KUHUSU KUGOMBANA NA WEMA SEPETU:
Baada ya siku chache za magazeti ya udaku nchini
kuripoti kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa karibu sana kati ya mwanadada
Wema sepetu na Muigizaji mwenzake Kajala masanja, tuliamua kufanya
uchunguzi wa kina ili kupata ukweli wa suala hili ili tusije kuipotosha
jamii kwa habari za zisizo na ushahidi wowote.
Katika habari iliyoripotiwa na blogs na magazeti kadhaa ya udaku
kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo zilisema kuwa chanzo ni vitendo vya
mwanadada wema Sepetu “kumbania” Kajala kwenye dili anzopata za kucheza
filamu na hasahasa kumkosesha dili ya kwenda china kufanya filamu
aliyoalikwa na watanzania waishio nchini humo.
Bongomovies.com tuliamua kuwatafuta hewani wasanii hawa ili
tuweze kupata ukweli wa jambo hili na mwanadada Kajala alikuwa wa kwanza
kupokea simu na alikanusha vikali habari hizo na kuwashangaa
wanaoziandika wanazipata wapi.
“Unajua mi nashangaa sana watu wanatoa wapi maneno wanayoandika,
mimi sina tatizo na Wema, wala siwezi kuwa na tatizo naye, wema amekuwa
msaada mkubwa kwangu, sa sijui nitagombana nini na wema, huo ni uzushi
tuu jamani, muwe mnatuuliza kabla ya kuandika” Alisema kajala
Alipoulizwa kuhusu ukaribu wake mpya na wolper alisema
“Wolper nimekutana naye kwenye party ndo tukaamua kupiga picha,
au siku hizi sitakiwi kupiga picha na mtu mwingine zaidi ya wema? Wolper
ni rafiki yangu” Alisisitiza Kajala
Tulipojaribu kumtafuta wema simu yake ilikuwa haipokelewi na baadaye ilipokelewa na alisema yuko location anatengeneza filamu na mwigizaji Rado hivyo tumtafute baadaye.
No comments:
Post a Comment