MAHAKAMA
Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela
askari saba wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma ambao walikuwa wakishtakiwa kwa
mauaji.
Akitoa hukumu
yake katika kikao cha Mahakama Kuu kilichokuwa kikifanyika mkoani Kigoma Jaji
wa mahakama hiyo, Sam Mpaya Rumanyika alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi
mbalimbali Mahakama hiyo imewatia hatiani askari hao kwa kosa la kuua bila
kukusudia.
Katika
kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012 washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo
na kusomewa shitaka la kumuua Festo Stephano, mkulima wa kijiji cha Rungwe Mpya
Wilaya ya Kasulu mkoani hapa katika tukio lililotokea Agosti 6, mwaka 2011.
Askari
hao waliohukumiwa ni pamoja na Baraka Hongdi, Koplo Mawazo, Koplo Swahib, D/C
Charles, D/C Shamsi, D/C Jerry na D/C Amrani ambao kwa pamoja walikana shitaka
lao katika kesi hiyo namba 35 ya mwaka 2012.
Akitoa
utetezi kabla ya hukumu hiyo wakili wa washitakiwa, Method Kabuguzi aliiomba
Mahakama kuwafutia shitaka washitakiwa hao na kuwaachia huru kwani wote bado
vijana na wameoa hivi karibuni.
Sambamba
na hilo Kabuguzi alisema kuwa askari hao walikumbwa na mkasa huo wakati
wakitekeleza jukumu lao la ulinzi wa taifa ambapo walimkamata mtuhumiwa wa
kutumia silaha na ndipo kifo kikatokea wakati wakitekeleza majukumu yao.
Source: http://www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment