Siku ya leo, CHADEMA mkoa wa Arusha walikuwa na ratiba muhimu ya Kutoa
sadaka ya shukurani kwa Mungu kwa kutembelea vituo vya watoto yatima na
wenye mahitaji muhimu na kuwapa misaada ya vitu mbalimbali na fedha
taslimu kufuatia baraka za Mungu kuwawezesha baadhi kunusurika kifo kwa
mabomu na pia kwa ushindi mnono.
Msafara wa CHADEMA ulikuwa na viongozi wa chama wakiongozwa na mwenyekiti wa chama Wilaya aliyewakilisha pia mkoa, pamoja na madiwani wapya bila kuwasahau viongozi wa BAVICHA na makamanda Ally Bananga na
Alphonce Mawazo.Msafara wa CHADEMA ulikuwa na viongozi wa chama wakiongozwa na mwenyekiti wa chama Wilaya aliyewakilisha pia mkoa, pamoja na madiwani wapya bila kuwasahau viongozi wa BAVICHA na makamanda Ally Bananga na
Vitu vyote walivyotoa msaada kama sadaka vimetokana na michango binafsi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA zikiwemo familia kadhaa zilizoamua kuungana na chama katika sadaka hiyo.
Vituo vilivotembelewa ni cha Abu-Abdurahaman Oprhanage Centre cha Mbauda ambacho kinapoke a watoto wa kuanzia miaka mitatu na Samaritan Village cha Moshono ambacho kinapokea watoto wachangakabisa kuanzia chini ya mwezi mmoja, na wengi ni wale wanaotupwa na wazazi wao vichakani au majalalani na kwenye mifuko mara baada ya kujifungua.
No comments:
Post a Comment